Karibu kwenye ShopManagement

Suluhisho Bora la Usimamizi wa Biashara

Subscribe kwenye YouTube yetu
Android Logo

Total Users:

Pakua Sasa

Vipengele Muhimu

Nani Anaweza Kutumia?

Mahitaji ya Mfumo

Ada ya Usajili

Malipo ya mara moja ya Tsh 25,000/= inajumuisha usanidi wa programu, miundombinu ya mtandao, na masasisho ya kila wakati. Usajili una Renew kila mwaka kwa gharama ile ile ili kuhakikisha upatikanaji usio katizwa wa mfumo, msaada, na masasisho, kuhakikisha kuwa mfumo wako wa usimamizi wa duka/Biashara unakuwa wa kuaminika na unafaa.

Jinsi ya Ku Download na Ku Install Programu ya ShopManagement
Fuata hatua hizi ili Ku Download na Ku Install programu ya ShopManagement kwenye kifaa chako cha Android au Kompyuta:
  1. Pakua/Download Faili ya APK: Baada ya kubonyeza kiungo, utaelekezwa kwenye Mega. Bonyeza kitufe cha Download ili kupakua faili ya APK.
  2. Wezesha Ku Install Kutoka Vyanzo Visivyojulikana: Kwa vifaa vya Android, hakikisha umewezesha Ku Install kutoka kwa vyanzo visivyojulikana kwa kwenda kwenye Mipangilio (Settings) > Usalama (Security) > Ruhusu Ufungaji Kutoka Vyanzo Visivyojulikana (Install from Unknown Sources).
  3. Fungua Faili ya APK: Fungua programu ya File Manager au Downloads, tafuta faili ya APK ya ShopManagement, na bonyeza ili kuanzisha ufungaji.
  4. Thibitisha na Sakinisha Programu: Utaonyeshwa dirisha la kuthibitisha ufungaji. Bonyeza Install ili kumaliza ufungaji.
  5. Fungua Programu: Mara baada ya kumaliza ufungaji, bonyeza Open ili kuanzisha programu na kuanza kuitumia.
Kwa kuwa Ume Install programu kutoka nje ya Play Store, hakikisha unafanya sasisho za mara kwa mara kupitia tovuti hii ili kuendelea kupata vipengele vipya na usaidizi.
Jinsi ya Kufungua Biashara au Duka katika Programu ya ShopManagement
Fuata hatua hizi ili kuunganisha biashara au duka lako kwenye programu au kuendelea na duka ambalo tayari linatambulikana na mfumo:
  1. Fungua Programu: Baada ya kupakua na kufunga programu, tafuta ikoni ya ShopManagement kwenye skrini yako ya simu na Bonyeza ili kuifungua.
  2. Chagua "Mpya" au "Inatambulika": Kwenye skrini kuu, utaona vifungo viwili: Mpya na Inatambulika. Bonyeza Mpya ikiwa unataka kutumia programu kwa biashara au duka ambalo halijawahi kusajiliwa kabla, au Inatambulika ikiwa biashara yako au duka tayari limetambulika kwenye mfumo.
  3. Bonyeza "Anza" (Kwa Mpya): Baada ya kuchagua Mpya, utaelekezwa kwenye ukurasa wa usajili. Bonyeza Anza ili kuendelea na mchakato wa kuanzisha biashara yako au duka.
  4. Jaza Taarifa Zako: Jaza taarifa zako zote kwa usahihi, ikiwa ni pamoja na jina la biashara, anwani, na maelezo mengine muhimu. Sehemu ya Msimbo wa Duka/Biashara itapatikana baada ya kumaliza malipo ya Tsh 25,000/=.
  5. Fanya Malipo: Malipo ya Tsh 25,000/= yatalipwa kwa namba ya simu +255 673 550 040 kwa jina ABDILAHI KHAMIS. Baada ya malipo, utapokea SMS kuthibitisha malipo yako.
  6. Thibitisha na Wasilisha: Ikiwa haukupokea SMS, tafadhali wasiliana kupitia WhatsApp kwa namba +255 673 550 040. Baada ya kujaza taarifa zote na kuthibitisha malipo, bonyeza Wasilisha ili kuendelea na usajili.
  7. Bonyeza "Inatambulika" (Kwa Duka au Biashara Iliyosajiliwa): Ikiwa biashara yako au duka tayari limejisajili, bonyeza Inatambulika ili kuendelea na mchakato wa kuungana na akaunti yako iliyopo.

  8. Jaza Taarifa Zako: Kama ilivyo kwa "Mpya", utahitajika kujaza taarifa zako kwa usahihi. Hakikisha unajaza jina la duka lako, anwani, na maelezo mengine ya biashara yako. Hii itasaidia kuthibitisha biashara yako na kuanzisha matumizi ya programu.
  9. Bonyeza "Wasilisha": Baada ya kujaza taarifa zote, bonyeza Wasilisha ili kuendelea na mchakato wa kuungana na biashara yako tayari iliyosajiliwa katika mfumo.
Dashibodi Kuu - Muhtasari wa Biashara yako
Dashibodi Kuu ni sehemu muhimu inayokupa muhtasari wa kifedha wa biashara yako kwa haraka. Itakusaidia kufuatilia maendeleo yako na kufanya maamuzi sahihi kuhusu uwekezaji, manunuzi, na faida yako.

    1. Salio la Sasa: Hii inaonyesha kiasi cha pesa kilichopo kwenye biashara yako kwa sasa. Inajumuisha pesa zote ambazo zinapatikana na ambazo zinatumika katika shughuli za biashara kwa wakati huu.

    2. Jumla ya Uwekezaji: Hii inaonyesha jumla ya kiasi cha pesa kilichotumika kwenye uwekezaji wa biashara. Inahusisha fedha ambazo umetoa kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza biashara yako, ikiwa ni pamoja na gharama za matumizi ya awali.

    3. Jumla ya Kutoka: Hii inaonyesha jumla ya pesa ambazo umetoa kutoka kwa biashara yako. Inaweza kuwa fedha ulizochukua kwa matumizi yako binafsi au fedha zilizoondolewa kwa madhumuni mengine kutoka kwenye biashara.

    4. Jumla ya Mauzo: Hii inaonyesha jumla ya pesa ambazo umepata kutokana na kuuza bidhaa au huduma zako. Inasaidia kujua kiasi cha fedha kilichozalishwa kutokana na mauzo yako ya bidhaa.

    5. Jumla ya Manunuzi: Hii inaonyesha kiasi cha fedha ulizotumia kununua bidhaa na huduma kwa ajili ya biashara. Ni tofauti na Jumla ya Uwekezaji kwa sababu Jumla ya Uwekezaji inahusisha pesa zote ulizotoa kutoka mfuko wako binafsi kwa biashara, wakati Jumla ya Manunuzi ni fedha ambazo biashara yako imejipatia na kuzitumia tena kununua bidhaa au huduma.

    6. Faida: Hii inaonyesha kiasi cha faida unachopata kutoka kwa biashara yako. Ni tofauti kati ya mapato yako (mauzo) na gharama zako (manunuzi na uwekezaji). Inakusaidia kujua kama biashara yako inapata faida au inapata hasara.

    7. Kukopesha: Hii inaonyesha kiasi cha pesa ulizokopa au ulizotoa kwa wateja yako au kwa biashara nyingine kama mkopo. Inaonyesha jumla ya fedha ulizoazima kutoka kwenye biashara yako.

    8. Asilimia ya Faida: Hii inaonyesha asilimia ya faida inayopatikana kutoka kwa biashara yako. Asilimia hii inachukuliwa kwa kulinganisha faida yako na jumla ya mapato ya biashara.

    9. Umewekeza: Hii inaonyesha kiasi cha pesa ambacho wewe binafsi umekiweka au kumwekeza kwenye biashara yako. Ni tofauti na Jumla ya Uwekezaji kwa sababu Jumla ya Uwekezaji inahusisha pesa zote zilizowekezwa na wamiliki wote wa biashara, wakati Umewekeza inaonyesha tu kiasi cha fedha ulizowekeza wewe binafsi.

    10. Umetoa: Hii inaonyesha kiasi cha pesa ambacho umekitoa wewe binafsi kutoka kwa biashara yako. Ni tofauti na Jumla ya Kutoka kwa sababu Jumla ya Kutoka inaonyesha fedha zote zilizoondolewa kutoka kwa biashara, lakini Umetoa inahusisha tu kiasi cha pesa ulichokitoa wewe binafsi.

Huduma - Sehemu ya Kurekodi Huduma na Matumizi ya Biashara yako
Sehemu hii hukuwezesha kufuatilia na kurekodi matumizi ya biashara yako kwa urahisi, kujua gharama za uboreshaji bila kuathiri mauzo, na kufanya maamuzi bora ya kifedha.

    1. Kulipa Kodi: Hii ni sehemu ambapo utaandika kodi yoyote uliyolipa inayohusiana na biashara yako. Hii ni sehemu muhimu kwa ajili ya kufuatilia matumizi yako ya kodi.

    2. Matengenezo ya Biashara na Uboreshaji: Hapa utaandika gharama za matengenezo yoyote uliyofanya kwenye duka lako au biashara yako, kama vile upigaji rangi wa maduka, kuboresha vifaa, au kurekebisha vifaa vilivyoharibika.

    3. Mali Isiyouzwa (Fixed Assets): Hii ni sehemu ambapo utaandika mali unazozinunua kwa ajili ya matumizi ya biashara yako lakini hutauza. Kwa mfano, ikiwa unamiliki duka la vifaa vya ofisi, na umenunua printer au mashine ya kopi, mali hizi zitarekodiwa hapa. Hizi ni mali muhimu kwa biashara yako lakini si za kuuza.

    4. Huduma Zinazohusiana na Bidhaa Unazouza: Katika biashara yako, kama unauza pilau na biryani, hutakua unununua pilau au biryani moja kwa moja. Badala yake, utaweza kununua vitu kama mchele, viungo, na mengineyo. Hizi zote ni sehemu ya huduma na matumizi ya biashara yako ambazo zinahusiana na bidhaa zako lakini si za kuuza moja kwa moja.

Sajili Mfanyakazi - ShopManagement
Sehemu hii inakuruhusu kuongeza wafanyakazi kwenye duka lako kwa kujaza taarifa sahihi. Cheo cha mfanyakazi ni muhimu kitakusaidi kudhibiti ruhusa katika utumiaju wa mfumo.

    1. Mfanyakazi (Worker):
    • Uza Bidhaa: Mfanyakazi anaweza kuuza bidhaa kwa wateja.
    • Ripoti Zilizoharibika: Mfanyakazi anaweza kutoa ripoti za bidhaa zilizoharibika.
    • Kopesha: Mfanyakazi anaweza kukopesha bidhaa.
    • Kurudisha Mkopo: Mfanyakazi anaweza kusimamia marudisho ya mikopo iliyotolewa.


    2. Meneja (Manager):
    • Yote anayoweza kufanya mfanyakazi, meneja anaweza pia kufanya.
    • Sajili Mfanyakazi kwa Workers only: Meneja anaweza kusajili wafanyakazi wapya katika mfumo.
    • Hariri Mfanyakazi: Meneja anaweza kuhariri au kubadilisha taarifa za wafanyakazi katika mfumo.


    3. Mmiliki (Owner):
    • Mmiliki ana ufikiaji kamili wa kila kipengele cha mfumo. Anaweza kufanya yote yafanywayo na mfanyakazi na meneja pamoja na haya yafuatayo:
    • Fanya Maamuzi ya Fedha: Mmiliki anaweza kutathmini na kuamua kuhusu fedha zote za biashara.
    • Hariri Vipengele Vyote: Mmiliki anaweza kuhariri au kubadilisha taarifa zote za biashara, wafanyakazi, na vipengele vingine vya mfumo.
    • Sajili Wafanyakazi Wote: Mmiliki anaweza kusajili wafanyakazi wote, ikiwa ni pamoja na wenye cheo cha Meneja na Mfanyakazi.
    • Fanya Mabadiliko Yote ya Mfumo: Mmiliki ana ruhusa ya kufanya mabadiliko yote ya mfumo, ikiwa ni pamoja na vipengele vya usalama, mipangilio ya mfumo, na taarifa za biashara.


    Kwa kufafanua majukumu na wajibu wa kila mfanyakazi kulingana na cheo chake, unaweza kuhakikisha kuwa biashara yako inaendeshwa kwa usalama na kwa ufanisi. Hii pia itakusaidia kudhibiti ni kazi gani mfanyakazi anaruhusiwa kufanya, kupunguza makosa au matatizo katika mfumo.

Hariri Mfanyakazi
Sehemu hii inakuruhusu kuona na kuhariri taarifa za wafanyakazi, pamoja na kusimamisha ufikiaji wa wale walioacha kazi au kufukuzwa.

    1. Kutazama Taarifa za Wafanyakazi:
    • Ona majina ya wafanyakazi wako, vyeo, na maelezo yao muhimu.
    • Kujua nani bado anaendelea kufanya kazi kwenye biashara yako.


    2. Kuhariri Taarifa:
    • Badilisha jina, cheo, au taarifa nyingine za mfanyakazi.
    • Kurekebisha makosa kwenye usajili wa mfanyakazi.


    3. Kusimamisha au Kuzuia Ufikiaji (Inactivate Employee):
    • Unapomsimamisha mfanyakazi, hatoweza tena kuingia kwenye mfumo.
    • Hii ni muhimu kwa wafanyakazi waliomaliza kazi au wale waliotolewa kazini.
    • Unaweza kumruhusu mfanyakazi kutumia mfumo tena ikiwa atarejea kazini.


    Faida za Kipengele hiki:
    • Hudhibiti vizuri wafanyakazi wako na taarifa zao.
    • Hakikisha usalama wa biashara yako kwa kuzuia wafanyakazi wa zamani kuingia kwenye mfumo.
    • Hifadhi kumbukumbu za wafanyakazi wa zamani kwa marejeo ya baadaye.


Jumuisha Bidhaa
Sehemu hii inakuruhusu kuongeza wafanyakazi kwenye duka lako kwa kujaza taarifa sahihi. Cheo cha mfanyakazi ni muhimu kitakusaidi kudhibiti ruhusa katika utumiaju wa mfumo.

    1. Ongeza Bidhaa Mpya:
    • Jaza taarifa muhimu za bidhaa kama vile:
    • Jina la Bidhaa (Mfano: Mchele, Sukari, Soda)
    • Bei ya Kununua (Gharama uliyotumia kununua bidhaa hiyo)
    • Kiasi (Stock) (Idadi ya bidhaa unayoingiza kwenye biashara)


    2. Bidhaa Zinazoingia Zinaweza Kuuza:
    • Baada ya kuongeza bidhaa, zinapatikana moja kwa moja katika sehemu ya "Uza Bidhaa".
    • Hakikisha umeongeza bidhaa zote muhimu kabla ya kuanza kuuza.


    3. Uhariri wa Bidhaa:
    • Unaweza kurekebisha jina, bei, au kiasi cha bidhaa zilizoingizwa awali.
    • Hii hukupa urahisi wa kusimamia bidhaa zako ipasavyo.


    Faida za Sehemu ya Jumuisha Bidhaa
    • Inahakikisha bidhaa zote zinapatikana kwenye mfumo kabla ya kuuzwa.
    • Inakusaidia kufuatilia bei ya kununua na kuuza kwa faida bora.
    • Inatoa urahisi wa kusimamia bidhaa zako ndani ya biashara.
    • Husaidia kuepuka makosa ya kuuza bidhaa ambazo hazijaingizwa kwenye mfumo.


Uza Bidhaa
Sehemu ya Uza Bidhaa inakuwezesha kuripoti mauzo ya biashara yako kwa haraka na kwa urahisi. Mfumo huu unafanya kazi kwa njia otomatiki ili kuhakikisha unapata hesabu sahihi bila makosa.

    1. Kuuza Bidhaa kwa Haraka:
    • Chagua bidhaa unayotaka kuuza kutoka kwenye orodha.
    • Ingiza kiasi cha bidhaa unayouza.
    • Mfumo utahesabu bei moja kwa moja kulingana na bei ya bidhaa hiyo.
    • Bonyeza "Uza", na mauzo yako yatarekodiwa mara moja.


    2. Uhesabuji wa Mauzo Moja kwa Moja:
    • Mfumo unahesabu jumla ya bei kulingana na kiasi cha bidhaa unayouza.
    • Ikiwa unampa mteja punguzo, mfumo utahesabu bei mpya kiotomatiki.
    • Unaweza kuona mapato yako papo hapo kwa siku hiyo.


    3. Hifadhi ya Mauzo:
    • Mauzo yote yanahifadhiwa kwenye mfumo kwa kumbukumbu za baadaye.
    • Unaweza kuona ripoti za mauzo kwa siku, wiki, au mwezi.
    • Inakupa mwonekano wa bidhaa zinazouzwa zaidi.


    Faida za Sehemu ya Uza Bidhaa
    • Hurahisisha mchakato wa mauzo kwa sekunde chache.
    • Hupunguza makosa kwa kufanya mahesabu kiotomatiki.
    • Hutoa ripoti sahihi za mauzo kwa ufuatiliaji bora wa biashara.
    • Husaidia kuboresha usimamizi wa hisa kwa kuona bidhaa zinazouzwa zaidi.


Ripoti Zilizoharibika
Sehemu ya Ripoti Zilizoharibika inakuwezesha kuripoti bidhaa ambazo zimeharibika au zina kasoro. Hii inasaidia kudhibiti hisa na kupunguza hasara zisizotarajiwa katika biashara yako.

    1. Kuripoti Bidhaa Zilizoharibika:
    • Chagua bidhaa kutoka kwenye orodha.
    • Ingiza kiasi cha bidhaa zilizoharibika.
    • Bonyeza "Ripoti" ili kuhifadhi taarifa hizo kwenye mfumo.


    2. Uhakiki wa Ripoti:
    • Orodha ya ripoti za bidhaa zilizoharibika inapatikana kwa uhakiki.
    • Unaweza kuchuja ripoti kwa tarehe, aina ya bidhaa, au sababu ya uharibifu.
    • Ripoti hizi zinaweza kutumika kufanya maamuzi sahihi kuhusu bidhaa.


    3. Uchambuzi wa Bidhaa Zinazoharibika Mara kwa Mara:
    • Mfumo utahifadhi data ya bidhaa zinazoharibika mara kwa mara.
    • Hii itasaidia kuchambua sababu za uharibifu na kutafuta suluhisho.
    • Inaweza kusaidia kubadilisha msambazaji au kuboresha uhifadhi wa bidhaa.


    Sehemu hii ni muhimu kwa kudhibiti hisa na kuepuka hasara zisizotarajiwa.

Hariri Zilizoharibika
Sehemu ya Hariri Zilizoharibika inakuruhusu kuthibitisha ikiwa bidhaa zilizoripotiwa kuwa mbovu ni kweli kabla ya kuziondoa kwenye orodha ya bidhaa zako. Hii inahakikisha kuwa hakuna makosa katika mfumo wako wa biashara.

    1. Kuhakiki Ripoti za Bidhaa Zilizoharibika:
    • Orodha ya bidhaa zilizoripotiwa kama mbovu itakuwa hapa.
    • Angalia tarehe ya kuripotiwa.
    • Chunguza ikiwa bidhaa imeharibika kweli au kuna makosa kwenye ripoti.


    2. Kuondoa Bidhaa Zilizothibitishwa Kuwa Mbovu:
    • Baada ya kuthibitisha kuwa bidhaa imeharibika, unaweza kuiondoa kutoka kwenye orodha ya bidhaa zinazouzwa.
    • Mfumo utaiondoa bidhaa hiyo kutoka sehemu ya kuuza lakini itahifadhi rekodi zake kwa marejeo ya baadaye.
    • Hii inahakikisha kuwa hakuna bidhaa mbovu zinazouzwa kwa wateja.


    3. Kurudisha Bidhaa Ikiwa Haikuharibika:
    • Ikiwa ripoti ilikuwa na makosa na bidhaa bado iko katika hali nzuri, unaweza kuirejesha kwenye orodha ya bidhaa zinazouzwa.
    • Hii inasaidia kuepuka upotevu wa bidhaa ambazo hazijaharibika kwa kweli.


    MUHIMU: Hakikisha unathibitisha kila ripoti kabla ya kuondoa bidhaa kutoka kwenye mfumo wako.

Kopesha - Kuripoti Bidhaa Zilizokopwa
Sehemu ya Kopesa inakuruhusu kuripoti bidhaa zilizokopwa na wateja au watu wengine, na pia kufuatilia taarifa za wateja hao. Hii inahakikisha kuwa unaweza kudhibiti bidhaa zako zilizokopwa na kuhakikisha kuwa zinarejeshwa kwa wakati.

    1. Kuripoti Bidhaa Zilizokopwa:
    • Ingiza bidhaa zilizokopwa pamoja na maelezo ya mteja au mtu aliyekopa.
    • Weka tarehe ya kutoa bidhaa na tarehe ya kurudisha.
    • Fuatilia bidhaa zinazohitajika kurudishwa kwa urahisi.


    2. Ufuatiliaji wa Wateja Waliokopa:
    • Orodha ya wateja waliokopa bidhaa itapatikana hapa.
    • Taarifa za bidhaa zilizokopwa na wateja wataonyeshwa kwa urahisi.
    • Fanya ufuatiliaji wa wateja ili kuhakikisha bidhaa zinarudishwa kwa wakati.


    3. Kurudisha Bidhaa Zilizokopwa:
    • Wateja wanaweza kurudisha bidhaa zilizokopwa kwa biashara yako.
    • Unapoona bidhaa zimerudishwa, unaweza kuziondoa kwenye orodha ya bidhaa zilizokopwa.


    MUHIMU: Hakikisha unafuatilia bidhaa zilizokopwa kwa usahihi ili kudhibiti biashara yako.

Kurudishwa Mikopo - Kurudishwa Fedha za Mkopo
Sehemu ya Kurudishwa Mikopo inahusisha kurejesha fedha zilizokopwa kutotka kwenye Bidhaa ulizokopesha. Baada ya kurejeshwa fedha hizo, unapaswa kubofya kitufe cha Rudisha na mfumo utasasisha taarifa za fedha zilizorejeshwa na kuongeza fedha hizo kwenye salio la biashara yako.

    1. Kudhibiti Fedha Zilizorejeshwa:
    • Baada ya kurejeshwa kwa fedha, bofya kitufe cha Rudisha.
    • Fedha zilizorejeshwa zitaongezwa moja kwa moja kwenye salio lako la biashara.
    • Hii itahakikisha usahihi na uwazi wa kurejeshwa kwa fedha zote.


    2. Ufuatiliaji wa Mikopo na Marejesho:
    • Orodha ya mikopo na hali ya kurejeshwa itakuwa wazi kwenye mfumo.
    • Utakuwa na uwezo wa kufuatilia fedha zilizokopwa na kurudishwa kwa urahisi.


    3. Kurudisha Fedha kwa Usahihi:
    • Fedha zitarekodiwa moja kwa moja kwenye salio la biashara yako bila makosa.
    • Hii itasaidia kufanya usimamizi wa mikopo kuwa rahisi na wa haraka.


    Hakikisha kurejesha fedha zilizokopwa kwa usahihi ili kuhakikisha usimamizi bora wa mikopo.